Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi mabaya ya dini sasa yaangaziwe: Balozi Koki

Matumizi mabaya ya dini sasa yaangaziwe: Balozi Koki

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki hii kumefanyika mjadala kuhusu stahamala na maelewano baina ya watu wa imani tofauti za kidini. Washiriki walikuwa viongozi wa dini mbali mbali pamoja na wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Kenya ambao walieleza uzoefu wao katika harakati za vita dhidi ya ugaidi wakati huu ambapo vinahusishwa na matumizi mabaya ya dini. Je nini uzoefu wa Kenya na katika mjadala huo wamejifunza nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Koki Muli Grignon ambaye hapa anaanza kwa kutanabaisha baadhi ya kile ambacho Kenya imepitia.