Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya vitisho vya Al Shabaab, mchakato wa kisiasa unaendelea Somalia

Licha ya vitisho vya Al Shabaab, mchakato wa kisiasa unaendelea Somalia

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Nicolas Kay amesema licha ya magaidi wa Al Shabaab kuendeleza vitisho dhidi ya wananchi, bado mchakato wa kisiasa wa kuunda serikali shirikisho unaendelea na hautositishwa.

Akizungumza katika mahojiano kwa njia ya simu na Idhaa hii kutoka Nairobi, Kenya, Balozi Kay amesema majadiliano yanaendelea miongoni mwa jamii na na kwamba mchakato..

(Sauti ya Kay)

Uko nyuma ya ratiba hatuko pale ambako tulitaka tuwepo na hatuko pale ambapo serikali ya Somalia au bunge walitaka wawepo, lakini kuna maendeleo makubwa katika malengo matatu ya kuwa na shirikisho, kupitia upya katiba na kuwa na serikali na taasisi za uwazi zaidi 2016.”