Wafanyakazi wa WFP waliotoka Sudan Kusini bado hawajapatikana

Wafanyakazi wa WFP waliotoka Sudan Kusini bado hawajapatikana

Wafanyakazi watatu wa misaada wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP waliotoka Sudan Kusini mwanzoni mwa mwezi huu bado whawajapatikana limesema shirika hilo.

Kwa mujibu wa WFP wafanyakazi hao walikuwa kwenye msafarara wa magari ya Umoja wa Mataifa yaliyokuwa yamebeba msaada kupeleka kwa maelfu ya watu walioathirika na vita kutoka Malakal kwenda Melut kwenye jimbo la Upper Nile wakati walioshuhudia wakisema wakajikuta katikati ya mapigano ya kijamii..

Licha ya juhudi za kuwasaka tangu walipotoweka April mosi hakuna mafanikio yoyote. George Fominyen ni afisa wa WFP Sudan Kusini

(CLIP YA GEORGE FOMINYEN)

Kutoweka kwa wenzetu watatu kumeongeza hofu ya usalama wa wafanyakazi katika eneo hilo, tunaendelea kufuatilia kupitia uongozi wa Juba, Malakal na  Akoka, lakini hatujafanikiwa kupata taarifa zozote na tunahofia usalama wa wafanyakazi wetu.”

Kuzorota kwa usalama kumewalazimisha wafanyakazi wa WFP kusitisha operesheni zake katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.