Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tujali dunia yetu kama mama anayetulea: Ban Ki-moon

Tujali dunia yetu kama mama anayetulea: Ban Ki-moon

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema tunategemea mama dunia kuishi jinsi mtoto mchanga anavyohitaji mama yake kwa kila kitu. Grace Kaneiya ana maelezo zaidi.

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Katika taarifa iliyotolewa leo, Ban amesema, mwaka huu wa 2015 ni fursa ya kubadili tabia za binadamu na jinsi ya kutumia rasimali wakti ambapo jamii ya kimataifa inatarajia kukubaliana juu ya malengo ya maendeleo endelevu na kufikia makubaliano ya tabianchi.

Hata hivyo, Katibu Mkuu ameongeza kuwa mabadiliko yanahitajika si tu kwa ngazi ya uongozi lakini pia ni kwa kila binadamu anatakiwa kuchukua hatua, hata ikiwa ndogo, ili kupunguza uharibifu wa mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Nikhil Chandavarkar ni afisa mawasiliano wa kitengo cha maendeleo endelevu katik a Umoja wa Mataifa analeza baadhi ya mambo ya kufanya kuepuka uharibifu wa sayari  dunia

(SAUTI YA NIKHILCHANDAVAR)

"Kwa kubadili namna tunavyoishi, kubadili namna tunavyotumia na kuzalisha, kutumia usafiri wa uma badala ya binafsi, na knunua malighafi zinazoweza kuhuishwa."