Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dawa mseto bado ni thabiti dhidi ya Malaria Tanzania:

Dawa mseto bado ni thabiti dhidi ya Malaria Tanzania:

Zaidi ya asilimia 93 ya watanzania wanaishi kwenye  maeneo ambayo yanawaweka hatarini kukumbwa na Malaria. Hata hivyo serikali ya Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua za kinga, tiba na utambuzi wa mapema ili kudhibiti kuenea kwa Malaria. Je ni hatua gani zimechukuliwa wakati huu wa kuelekea siku ya Malaria duniani tarehe 25 Aprili.? Assumpta Massoi wa idhaa hii amezungumza na Dkt. Renata Mwandike, Naibu Meneja wa mpango wa kitaifa wa kudhibiti Malaria nchini humo ambapo hapa ameanza kwa kuelezea matokeo ya utafiti kuhusu maambukizi ya Malaria miongoni mwa watoto.