Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awa na mazungumzo na Rais Poroshenko wa Ukraine

Ban awa na mazungumzo na Rais Poroshenko wa Ukraine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Petro Poroshenko wa Ukraine kuhusu mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema katika mazungumzo hayo, Ban na Rais Poroshenko wamekubaliana kutekeleza kwa ukamilifu vipengele vyote vilivyomo katika makubaliano ya Minsk.

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuzingatia vipengele vyote vya kisiasa ili kuimarisha hali ya kibinadamu.

Kuhusu ujumbe wa kimataifa wa kulinda amani, Ban amesema hilo ni jambo la kuamuliwa na Baraza la usalama.

Katibu Mkuu amesisitiza usaizidi na mshikamano wa Umoja wa Mataifa na wananchi wa Ukraine katika kipindi hiki kigumu na kwamba wameazimia kuendeleza ushiriki wa umoja huo kwenye suala la Ukraine.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa tangu kuanza kwa mzozo wa Ukraine, zaidi ya watu Milioni Mbili wamepoteza makazi yao na kati yao hao Laki Nane wamekimbilia nchi jirani.