Skip to main content

Zahma ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediteranea

Zahma ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediteranea

Idadi ya waliofariki dunia kwenye bahari ya Mediteranea wakisaka hifadhi Ulaya kutoka Afrika tangu mwanzo wa mwaka huu ni mara kumi kulingana na idadi ya waliofariki dunia katika kipindi kama hicho mwaka jana , kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR.

Ongezeko hilo linatangazwa wakati watu kutoka Eritrea, Somalia, Syria, Libya na nchi mbali mbali za Afrika na Mashariki ya Kati wanazidi kujaribu kufunga safari hiyo hatari ya kuvuka bahari ya Mediteranea, ajali na mateso huongezeka. Wiki iliyopita, serikali ya Italia pamoja na UNHCR zimeokoa wahamiaji 70 ambao walikuwa wanazurura kwenye bahari.

Wengi wao waliunguzwa na moto baada ya mtungi wa gesi kulipuka. Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.