Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani mauaji ya wakristo kutoka Ethiopia huko Libya

Baraza la usalama lalaani mauaji ya wakristo kutoka Ethiopia huko Libya

Wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali  mauaji ya kikatili ya zaidi ya waethiopia 30 wa madhehebu ya kikristo huko Libya yaliyofanywa na washirika wa magaidi wa ISIL au Da’esh.

Katika taarifa yao, wajumbe hao wamesema kitendo hicho cha uhalifu kwa mara nyingine kinadhihirisha ukatili unaofanywa na magaidi hao wa ISIL dhidi ya raia wa madhehebu mbali mbali ya dini, makabila na utaifa huku wakipuuuza thamani ya ubinadamu.

Wamerejelea wito wao wa kulaani vikali mauaji ya binadamu kwa misingi ya imani zao za kidini.

Halikadhalika wamesisitiza ushindi dhidi ya ISIL lazima na kwamba ukosefu wa stahamala, ghasia na chuki ambavyo kikundi hicho kinaeneza ni lazima vitokomezwe.