Uwekezaji dhidi ya Malaria umeokoa maisha Tanzania:

Uwekezaji dhidi ya Malaria umeokoa maisha Tanzania:

Kuelekea siku ya Malaria duniani tarehe 25 mwezi huu, Tanzania imesema uwekezaji katika kinga, tiba na ugunduzi wa mapema wa ugonjwa huo umesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo ikotolea mfano kwa watoto wadogo.

Naibu Meneja wa mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria nchini humo Dkt. Renata Mandike ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa usambazaji wa vyandarua vyenye viuatilifu, dawa mseto na mifumo bora ya utambuzi wa Malaria imewezesha idadi ya watoto wanaougua Malaria kupungua kwa asilimia 40 mwaka 2012.

(Sauti Dkt, Mandike)

Wakati ujumbe wa mwaka huu unataka serikali kuwekeza ili kutokomeza Malaria, kwa mujibu wa Dkt, Mandike Tanzania inajenga kiwanda cha kuimarisha kinga dhidi ya Malaria.

(Sauti ya Dkt. Mandike)

Kwa mujibu wa Dkt, Mandike kiwanda hicho kinachojengwa Kibaha mkoa wa Pwani kiko katika hatua za mwisho wa ujenzi na kitaongeza jitihada za kutokomeza Malaria kwenye nchi hiyo ambayo asilimia 93 ya wananchi wake wako hatarini kukumbwa na Malaria kutokana na jiografia yake.