Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa kidini wajadili stahamala ili kutokomeza msimamo mkali

Viongozi wa kidini wajadili stahamala ili kutokomeza msimamo mkali

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, wajumbe wa nchi wanachama wamekutana na viongozi wa kidini kwa ajili ya mjadala maalum wa siku mbili kuhusu stahamala na maridhiano. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mjadala huu, Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa amesisitiza umuhimu wa mawasialiano baina ya watu wa imani tofauti za dini ili kutokomeza msimamo mkali, ugaidi na ubaguzi duniani, akizingatia jukumu la viongozi wa kidini katika kueneza ujumbe wa stahamala na mshikamano kwa jamii.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni muhimu kukabiliana na mizizi ya hatari ya vikundi venye msimamo mkali kama vile Boko Haram, Da’esh au Al Shabaab, ambavyo ni kizazi kipya cha magaidi kinachohatarisha usalama na amani ya kimataifa.

Bwana Ban ameeleza kwamba Umoja wa Mataifa unatarajia kuunda mpango maalum wa kuzuia msimamo mkali.

“ Mkakati wa Umoja wa Mataifa utazingatia maadili ya misingi ya amani, haki na utu kama njia mbadala dhidi ya ukatili wa vikundi venye msimamo mkali. Utalenga kinga kupitia mamlaka za serikali zenye usawa, utawala jumuishi, na heshima kwa haki za binadamu na utawala wa sheria.”