Skip to main content

Mpango wa EU kunusuru wahamiaji huko Mediterranean, UNHCR yawa makini

Mpango wa EU kunusuru wahamiaji huko Mediterranean, UNHCR yawa makini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekaribisha huku ikichukua hadhari mpango wa Muungano wa Ulaya, EU wa kuzuia wahamiaji kuzama baharini Mediterranean wakati wa safari zao za kusaka maisha bora barani humo. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Akizunguzma na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo, msaidizi wa Kamishna Mkuu wa UNHCR kuhusu ulinzi Volker Turk amesema mpango huo wenye vipengele 10 ni mwanzo mzuri lakini umejikita zaidi katika kushughulikia wasafrishaji haramu badala ya wahamiaji ambao maisha yao yako hatarini.

Mathalani amesema wametaja upatiaji makazi, usaidizidi wa Ulaya kwa Italia na Ugiriki lakini bado kinachohitajika ni mipango ya kina kuhusu mwelekeo wa kisheria kuhusu uhamiaji, usaidizi wa kibinadamu na jinsi ya kukidhi mahitaji ya wakimbizi wanapowasili barani humo.

EU ilitangaza mpango huo Jumatatu baada ya watu 800 waliondoka Libya mwishoni mwa wiki kuzama baharini.

Kwa mujibu wa manusura waliohojiwa na UNHCR, wahamiaji 350 walitoka Eritrea ilihali wengine wametoka Syria, Somalia, Sierra Leone, Mali, Senegal, Gambia, Ivory Coast na Gambia.