Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa Ulaya uchukue hatua dhidi ya vifo vya wahamiaji baharini:Zeid

Muungano wa Ulaya uchukue hatua dhidi ya vifo vya wahamiaji baharini:Zeid

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein ataka Muungano wa Ulaya wakubali kwamba wanahitaji wafanyakazi wahamiaji.  Tamko hilo limekuja kufuatia vifo vya wahamiaji 700 waliozama bahari ya Mediteranian mwishoni mwa wiki.

Katika taarifa yake ya Jumatatu , Kamishina mkuu Zeid Ra'ad Al Hussein amesema hakushangazwa bali ametishwa  baada ya kubaini kwamba watu wengine wanaume , wanawake na watoto wamefariki dunia katika kutafuta maisha bora ng’ambo.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayeamua kuchukua safari hiyo ya hatari kama angekuwa na hiyari ya kuchagua.