Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa usaidizi wa kibinadamu lazima ubadilike: Ban

Mfumo wa usaidizi wa kibinadamu lazima ubadilike: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuelekea katika mkutano kuhusu misaada ya kibinadamu nchini Uturuki mwezi Mei, matarajio ni kuzidisha msaada wa kimataifa katika kuleta mabadiliko katika usaidizi wa kibinadamu.

Akihutubia mkutano wa awali hapa mjini New York Bwana Ban amewaeleza wawakilshi wa nchi mablimbali kuwa ni lazima kubadili mfumo wa usaidizi wa kibidanamu kwa kuwa

(SAUTI BAN)

"Dunia inabadilika, na tunahitaji kubadilika ili kuayatimiza mahitaji ya waathiriwa wa mizozo kwa wakati na kwa ufanisi."

Amesema idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka 10 ambapo zaidi ya watu milioni 51 hawana makazi duniani.

Kati yao watoto ni sehemu ya waathiriwa ambapo wengine wameshindwa kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa.