Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani vikali mauaji ya waethiopia nchini Libya:

Ban alaani vikali mauaji ya waethiopia nchini Libya:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya kikatili dhidi ya raia kadhaa wa Ethiopia yanayofanywa na watu wanaohusiana na kundi la Daesh nchini Libya.

Ameshutumu ulengaji wa watu kwa misingi ya kidini na Imani zao. Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi  kwa familia zilizopoteza maisha na kwa serikali ya Ethiopia kutokana na vitendo hivyo vya kikatili.

Ban ameendelea kusistiza kuwa mazungumzo yanayowezeshwa na Umoja wa Mataifa  ni fursa pekee kwa Walibya kukabiliana na mgogoro unaoendelea nchini humo.

Amezichagiza pande zote husika kuchukua hatua zozote zinazohitajika kufikia muafaka.  Amesema kwa kufanya kazi pamoja pekee ndio kutawawezesha Walibya kuanza ujenzi mpya wa taifa na taasisi ambazo zitaukabili ugaidi.