Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wanne wa UNICEF wauawa Garowe Somalia

Wafanyakazi wanne wa UNICEF wauawa Garowe Somalia

Wafanyakazi wanne wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamearifiwa kuuawa kwenye shambulio  dhidi ya gari walilokuwa wakisafiria mjini Garowe Somalia. Taarifa ya  Grace Kaneiya inafafanua Zaidi.

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

Wafanyakazi wengine waliojeruhiwa wameripotiwa kuwa katika hali mbaya.. Shambulio hilo limetokea wakati wafanyakazi hao walipokuwa wakisafiri kutoka kwenye nyumba ya kulala wageni wanayoishi kuelekea ofisini ambapo kwa kawaida ni safari ya dakika tatu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake shambulio hilo la kinyama sio tuu dhidi ya wafanyakazi wa UNICEF bali pia ni kwa watu wanaosaidiwa na shirika hilo.Edward Cwardine ni naibu Mkurugenzi wa mawasiliano UNICEF

("Kuendelea kufanya kazi kwa watoto na familia katika mazingira magumu ndiyo kipaumbele, na tutaendelea kadri tuwezavyo.")

Ameongeza kuwa wafanyakazi hao walijitolea maisha yao kufanya kazi kwa ajili ya kusaidia watoto wa Somalia, sio wahanga bali pamoja na waliojeruhiwa ni mashujaa. UNICEF hivi sasa inawasiliana na familia za wafanyakazi hao na kusafirisha majeruhi.

Pia shirika hilo na mkurugenzi wake mkuu wametuma salamu za rambirambi kwa wafanilia na jamaa wa waliopoteza maisha na kuwatakia nafuu ta haraka majeruhi.