Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pandeni mbegu kwenye agenda ya maendeleo endelevu: Ban

Pandeni mbegu kwenye agenda ya maendeleo endelevu: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema watu ndio kitovu cha  agenda mpya ya maendeleo endelevu.

Akiongea mjini Washinton Dc mwishoni mwa juma wakati wa kamati ya kimataifa ya   fedha, Bwana Ban amesema kuwa agenda ya maendeleo ni maono ya dunia hivyo kutaka viongozi wa  taasisi za uma za kifedha kupanda mbegu katika maono hayo.

Amesema wanufaika wakuu ni raia na kuongeza kuwa maono hayo yatawezesha ukuaji wa kiuchumi, mabadiliko katika mazingira na hata maendeleo ya kijamii.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa lengo kuu katika agenda ya maendeleo endelevu ni kuondoa umaskini na mafaniko ya pamoja, akisisitiza kuwa utekelezaji mwema wa mpango huu utakuwa kichocheo cha uchumi ambao ni endelevu na wenye uwiano.

Katika kuchukua hatua Ban amesema Umoja wa Mataifa umeandaa mkutano maalum mnamo tarehe 25 hadi 27 mwezi Septemba ambapo viongozi wa dunia watapitisha agenda mpya ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yennye shauku na shirikishi ambayo itaitwa SDG ikichukua nafasi ya yale yanayofikia ukomo yaani maleongo ya maendeleo endelevu MDGS