Skip to main content

Baraza la usalama lasisitiza amani Burundi ikielekea uchaguzi

Baraza la usalama lasisitiza amani Burundi ikielekea uchaguzi

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamevitaka vyama vya siasa nchini Burundi kuilinda amani ya Burundi ili kuepusha nchi kutumbukia katika machafuko wakati huu ambapo taifa hilo linaelekea katika uchaguzi.

Tamko la baraza hilo lilofuatia kikao cha April 16 linasema uchaguzi unaokuja ni tukio nyeti ambalo ikiwa halitaangaliwa  kwa umakini laweza kuchochea machafuko na kuitowesha amani iliyodumu kwa takribani muongo mmoja chini ya makubaliano ya Arusha.

Wajumbe wa baraza wamekaribisha kujihusisha kwa  Katib Mkuu Ban Ki-Moon, Kamishna mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein, na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete katika kuhakikisha uchaguzi wa amani na utulivu.

Baraza pia limeunga mkono tamko la Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein lililoeza kusikitishwa na kukua kwa mvutano na kutaka serikali na vikozi vya usalama kutuliza vuguvugu la kundi liitwalo  Imbonerakure. Tamko hilo pia limetaka upinzani na vikundi wafuasi kuhakikisha amani..

Tamko hilo pia lilitaka amani vyama vyote kujiepusha na matamshi ya chuki, na aina zote za machafuko na majibishano yanayoweza kuleta hofu. Wamelaani pia jaribio la kutaka kumuua mke wa kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa.