Skip to main content

Takwimu pekee hazitoshi, tunataka tujumuishwe: Mwanaharakati kijana

Takwimu pekee hazitoshi, tunataka tujumuishwe: Mwanaharakati kijana

Mkutano wa 48  kuhusu idadi ya watu na maendeleo ulioandaliwa  na tume ya idadi na maendeleo CPD umekamilika leo hapa New York . Makundi mablaimbai ya wadau wa maendelo wamejadili namana wanavyoweza kukuza maendeleo kwa kuzingtia ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Miongoni mwa makundi yaliyowakilishwa katika mijadala kupitia mkutano huu ni vijana kundi ambalo linataka kuwakilishwa katika mpango wa maendeleo endelevu. Brenda Mbaja ni mwanaharakati kijana na mwakilishi wa mtandao wa barubaru na vijana wa Afrika NAYA kutoka Kenya na katika mahojiano kandoni mwa mkutano huo amemweleza Joseph Msami wa idhaa hii kuwa takwimu hazitoshi kuwajumuisha vijana na kutaka wapewe fursa timilifu.

Kwanza  anaanza kwa kueleza hasa wanajadili nini katika muktadha wa vijana.

(SAUTI MAHOJIANO)