Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yahitaji dola milioni 30 kusaidia wakimbizi kambini Yarmouk

UNRWA yahitaji dola milioni 30 kusaidia wakimbizi kambini Yarmouk

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linatafuta fedha za dharura kiasi cha dola za kimarekani milioni 30 kwa ajili ya kutoa msaada kwa raia 18,000 katika kambi ya wakimbizi Yarmouk, miongoni mwao wakiwa watoto 3,500 pamoja na wengine walioathiriwa na mgogoro na kupoteza makazi katika maeneo mengine.

Taarifa ya UNRWA inasema kuwa msaada huu wa siku 90 pia unalenga usaidizi kwa ajili wakimbizi wa Palestina 480,000 walioko Syria na wasio na makazi nchini Lebanon na Jordan.

Mkuu wa UNRWA nchini Syria Michael Kingsley amesema hali ni tete kufuatia machafuko katika ukanda huo na kutaka mwitikio wa haraka kwa wahitaji.

Katiak siku za hivi karibuni UNRWA imesogeza ugawaji wa misaada katiak maeneo jirani na kambi ya Yarmouk ambapo wengi wa raia wanahitaji malazi huku pia ikigawa vyakula, huduma za kiafya, mablanketi, na huduam za kujisafi.