Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukarabati wa vurugu za wahalifu wenye msimamo mkali ni muhimu saana nchini Nigeria:Dr.Agomoh

Ukarabati wa vurugu za wahalifu wenye msimamo mkali ni muhimu saana nchini Nigeria:Dr.Agomoh

Ukarabati wa vurugu zinazofanywa na watu wenye msimamo mkali nchini Nigeria ni muhimu saana kwa hivi sasa wakati taifa hilo likikabiliwa na changamoto kubwa na wanamgambo na kundi la Boko Haram.

Hayo yamesemwa na Dkt. Uju Agomoh Mmkurugenzi mtendaji wa wa hatua za urekebishaji na hali ya magereza (PRAWA) wa Nigeria alipozungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa kukabiliana na uhalifu unaoendelea Doha Qatar.

(SAUTI YA DKT. UJU AGOMOH)

“Ni muhimu saana kwa sababu unapomkamata mhalifu , gaidi kuhakikisha kuna mambo yanayofanyika kupunguza fursa ya mtu huyo kufanya tena uhalifu. Sio hilo tuu bali pia unapunguza fursa za mtu huyu kufanya makosa na  kuwarubuni wengine, unataka kuhakikisha kwamba kwa hatua za utekelezaji kweli unazuia. Sababu usipokuwa makini utakuwa kwamba mtazamo unaochukua unaweza kuongeza idadi ya wanamgambo au magaidi jambo ambalo hakuna nchi inalitaka.

Dkt. Agomoh ameongeza kuwa hili ni tatizo la kimataifa na sio la nchi kadhaa.