Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mpoko CAR kufungwa Mei:OCHA

Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mpoko CAR kufungwa Mei:OCHA

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR imetangaza kuwa eneo kubwa la Mpoko lililopo kwenye uwanja wa ndege ambalo linahifadhi wakimbizi wa ndani litafungwa mwishoni mwa mwezi Mei.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala  ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA eneo hilo linahifadhi wakimbizi wa ndani 10,300 hivi sasa lakini wakati machafuko yaliposhika kasi mwaka jana lilikuwa na wakimbizi wa ndani 100,000.

OCHA imesema timu yake nchini humo itasaidia kuwahamisha wakimbizi hao wa ndani kwa lengo la kuwajumuisha tena katika jamii zao.