Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya wahamiaji vyaongezeka Mediterranean:IOM

Vifo vya wahamiaji vyaongezeka Mediterranean:IOM

Wakati idadi ya wahamiaji wanaookolewa na kuwasili Kusini mwa Italia inaongezeka timu ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inaendelea kukusanya ushahidi wa takribani watu 400 wanaodaiwa kufa maji mapema wiki hii.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa IOM ofisi ya uratibu Mediteraniani Federico Soda , wakati idadi ya watu wanaowasili mwaka huu ni sawa na ile iliyoorodheshwa katika wakati kama huu mwaka jana, idadi kubwa ya wanaowasili katika siku chache ni ya kawaida.

Majeshi ya wanamaji ya Italia yameendesha operesheni za ukozi kwa wahamiaji waliokuwa katika hali mbaya katika bahari ya Mediterania siku nzima ya Alhamisi na kuwafikisha katika badari za Augusta na Trapani, ambako kwa siku hii tu wameandikishwa wahamiaji 600 Augusta na 580 Trapan.