Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yalaani vikali mashambulizi yaliyouwa raia , Beni DR Congo

MONUSCO yalaani vikali mashambulizi yaliyouwa raia , Beni DR Congo

Mwakilishi na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO, Bwana Martin Kobler amelaani vikali na kusema ameshitushwa na mauaji ya raia karibu na eneo la Beni nchini humo. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Taarifa ya MONUSCO imemnukuu Kobler akisema ni muhimu kwa jeshi la serikali FARDC na MONUSCO kuanza tena operesheni zake , kwani kwa pamoja itawezekana kuepuka kuzorota zaidi kwa hali ya usalama.

Mashambulizi hayo yanayoshukiwa kufanywa na kikundi cha ADF yametokea kilometa 5 Kaskazini Mashariki mwa Mbau mjini Beni kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Bwana Kobler ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa mashambulizi hayo ya asubuhi ya leo.