Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa hofu na ghasia za chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini

UNHCR yatiwa hofu na ghasia za chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini

Mashambulizi yatokanayo na chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini yamekatili maisha ya watu 6 na kusambaratisha raia 5000 wa kigeni, wakimemo wakimbizi, na waomba hifadhi kwenye jimbo la Mashariki la Kwazulu-Natal katika wiki tatu zilizopita.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema linatiwa hofu na mashambulizi hayo yaliyoanza mwishoni mwa mwezi Machi kufuatia mgogoro unaohusiana na ajira ukiwahusisha raia wa kigeni na wenyeji wa Afrika Kusini. Hali kama hii ilijitokeza pia mwezi Januari katika maeneo ya Soweto, karibu na Johannesburg jimbo la Guateng.

UNHCR imepeleka timu mjini Durban kutathimini hali halisi na kuona ni jinsi gani inaweza kuisaidia serikali na jumuiya za kijamii kukabiliana na hali hii wakati huu ambapo mabalozi wa nchi za Afrika wakikutana kama anavyoeleza Elibahati Lowassa kaimu balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini

(SAUTI LOWASSA)

Raia wa kigeni 1400 wameshapatiwa hifadhi huku wengine 1500 wakihamishwa jana pekee .