Tunachukua hatua kupunguza urasimu unaokwamisha ukuaji uchumi:Tanzania
Tanzania inaendelea kuchukua hatua kuboresha mazingira ya biashara kwenye sekta ya umma, ikiwa ni mojawapo ya harakati za marekebisho ya kimuundo ili kuchangia ukuaji uchumi.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Saada Mkuya Salum amesema hayo alipohojiwa na Idhaa hii kando mwa vikao vya msimu wa chipukizi vya benki ya dunia vilivyoanza huko Washington DC wakati huu ambapo Benki hiyo imeshauri nchi kufanya marekebisho ya kimuundo kama njia ya kukuza uchumi.
Amesema tayari wamepitisha muswada wa sheria wa kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na afya lakini…
(Sauti ya Saada)
Kuhusu ushauri wa Benki ya dunia wa kutaka nchi ziwekeze kwa rasilimali watu, Waziri huyo wa Fedha ametolea mfano wa mradi wa matokeo makubwa sasa akisema umekuwa na mafanikio kwenye elimu na hata kwenye maji...
(Sauti ya Saada)
Kwa mujibu wa Waziri Saada, awamu ya pili ya mradi wa matokeo makubwa sasa, BRN pamoja na mambo mengine itaangazia afya.