Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kufanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Marekani

Ban akutana na kufanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Marekani

Akiwa Washington DC Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter na kushukuru mchango wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa husuani katika ulinzi wa amani kupitia vikosi katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa sehemu mbalimbali duniani.

Katibu Mkuu amejadili na waziri huyo wa ulinzi kuhusu maandalizi ya mkutano wa mwaka 2015 kuhusu mageuzi ya ulinzi wa amani. Viongozi hao pia wamezungumzia vikosi vya Umoja wa Mataifa vya ulinzi wa amani sehemu mbalimbali duniani ikiwamo Haiti, Mali, Sudan Kusini, . Kadhalika wamejadili hali nchini Yemen.