Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia Afrika Kusini dhidi ya wahamiaji, UM wazungumza

Ghasia Afrika Kusini dhidi ya wahamiaji, UM wazungumza

Umoja wa Mataifa umezungumzia ghasia zinazoendelea huko Afrika ya Kusini dhidi ya wageni na kutaka serikali zihakikishe sheria kuhusu wahamiaji zinakidhi vigezo vya kimataifa.

Msemaji wa Umoja huo Stéphane Dujarric ameeleza hayo alipoulizwa na waandishi wa habari jijini New York kuhusu matukio hayo akisema hawezi kuelezea chanzo chake  au arejelee historia lakini wakati wa machungu ya kiuchumi, wahamiaji ndio walengwa wa kwanza, lakini jambo muhimu ni kwamba..

(Sauti ya Dujarric)

“Wahamiaji wana haki wanapaswa kulindwa, serikali zinapaswa kuhakikisha sheria zinakidhi viwango vya kimataifa na sababu hasa za mivutano hiyo ni  vyema zikashughulikiwa na kama watu wana malalamiko nayo yapatiwe suluhu kwa amani. ”

Amesema wahamiaji ni kundi ambalo liko hatarini iwe Afrika Kusini, baadhi ya maeneo ya Ulaya na maeneo mengine duniani na matukio ya kuwalenga yamekuwa yakiongezeka.