Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA na Iran wamejadili muendelezo wa utekelezaji wa mpango wa ushirikiano

IAEA na Iran wamejadili muendelezo wa utekelezaji wa mpango wa ushirikiano

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic  IAEA na serikali ya Iran, wamekuwa na mkutano wa kiufundi jana April 15 mjini Tehran.

Pande hizo mbili zimejadili muendelezo wa utekelezaji wa mpango wa ushirikiano katika masuala ya nyuklia. Na wamekuwa na mjadala mzuri kuhusu hatua mbili kubwa zilizokuwa kwenye ajenda.

IAEA na Iran wataendelea na mazungumzo na wameafikiana kukutana tena hivi karibuni.