Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ichukue hatua hima chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini: IOM

Serikali ichukue hatua hima chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini: IOM

Kufuatia matukio ya hivi karibuni ya  chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini, yaliyosababisha vifo vya watu sita, 100 kujeruhiwa na wengine takribani 3000 kukosa makazi , Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) nchini humo limeitaka serikali kuunda chombo cha kukabiliana na machafuko na kuwafikisha watekelazaji wa vitendo  hivyo katika vyombo vya sheria.

Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa kutoka nchini humo mkuu wa IOM Richard Ots amesema lazima mtizamo hasi dhidi ya wahamiaji ubadilike na akataja kile ambacho IOM inafanya ikiwa ni hatau za dharura.

(SAUTI RICHARD )

Tunachokifanya ni kuweka mfumo wa kuwarejesha makwao waathiriwa wakiwmo majeruhi wanaotaka kurejea katika nchi zao , pia tunafuatailia kwa karibu hali livyo na kuipa taarifa serikali juu ya maedeleo ya  machafuko