Skip to main content

Heko Tume ya ujenzi wa amani kwa usaidizi wakati wa Ebola: Kutesa

Heko Tume ya ujenzi wa amani kwa usaidizi wakati wa Ebola: Kutesa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema Tume ya ujenzi wa amani ya Umoja huo na mfuko wa ujenzi wa amani ni muhimu zaidi wakati huu ambapo harakati za ujenzi wa amani endelevu zinapaswa kuimarishwa zaidi hasa baada ya majanga na mizozo.

Akifungua mjadala wa pamoja kuhusu ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mfuko na tume hiyo, Kutesa ametolea mfano vile ambavyo mlipuko wa Ebola ulitishia matunda ya amani, usalama  na maendeleo yaliyokuwa yamepatikana baada ya jitihada kubwa huko Liberia, Sierra Leone na Guinea, hivyo akasema..

(Sauti ya Kutesa)

 “Napongeza tume ya ujenzi wa amani kwa jitihada zake na msaada wake kwa nchi zilizoathirika na  nashukuru nchi wanachama kwa mshikamano walioendelea kuonyesha na nchi za Afrika Magharibi. Napongeza pia serikali za nchi zilizoathirika zaidi kwa hatua walizochukua haraka kudhibiti mlipuko huo.”