Ushirika wa sekta binafsi na za umma kukabiliana na uhalifu wa kupangwa katika mitandao:

Ushirika wa sekta binafsi na za umma kukabiliana na uhalifu wa kupangwa katika mitandao:

Wakati kila siku kuna picha zaidi ya bilioni 1.8 zinazowekwa na kusabazwa kwenye mitandao ya intaneti imekuwa rahisi sana kukuta picha za ngono zinazohusisha watoto umesema mkutano wa kukabiliana na uhalifu unaonedelea Doha Qatar.

Hata hivyo nyenzo mpya iliyoanzishwa na kutolewa bure na kampuni ya kompyuta ya Microsoft kwa vyombo vya sheria , huenda hali ikabadilika hivi karibuni.

Washiriki kwenye mkutano huo wa Doha wameambiwa kuwa changamoto ya uhalifu wa mtandao ni kubwa kuliko inavyodhaniwa na ili kukabiliana nayo ni lazima kuwe na ushirikiano wa karibu baina ya sekta za umma na binafsi. Dale Waterman ni kiongozi wa Microsoft wa kitengo cha uhalifu wa kimtandao kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika.

(SAUTI YA DALE WATERMAN)

“Ushirika baina ya sekta binafsi za umma ni muhimu saana . tatizo ni kubwa sana na hakuna njia yoyote ambapo chombo kimoja tu kinaweza kukabiliana nalo, na ndio maana Microsoft tutakuwa tunafanya kazi na vyombo vya sheria , na sekta za benki, kwa sababu unahitaji ushirikiano wa kila muhusika kuhakikisha kwamba tunaleta mabadiliko."