Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya raia wa Yemen wanakabiliwa na hatari ya usalama wa chakula: FAO

Mamilioni ya raia wa Yemen wanakabiliwa na hatari ya usalama wa chakula: FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema wakati machafuko yakiendelea nchini Yemen watu takriban milioni 11 wanakabiliwa na uhaba wa chakula huku mamilioni wengine wakiwa katika hatari ya kutotimiza mahitaji ya msingi ya chakula.

Hii ni kwa mujibu wa tathmini ya karibuni ya usalama wa chakula iliyotolewa na FAO.

Ripoti hiyo pia inaashiria kwamba karibu watu milioni 10.6 nchini Yemen hivi sasa wanakumbwa na uhaba wa chakula karibu katika miji yote kutokana na machafuko yaliyosababisha bei za chakula kupanda na kuingilia uzalishaji wa kilimo.

Watu wapatao milioni 16 kati ya milioni 26 ambao ni idadi ya watu wote nchini Yemen wanahitaji msaada wa kibinadamu na hawana maji safi. Salah El Hajj Hassan ni mwakilishi wa FAO Yemen

“ Katika maeneo kadhaa, na majimbo kadhaa ya YEmen, kulikuwa na maghala kwa ajili ya kuhifadhi ngano, kwa mfano, ambayo inaingizwa kutoka nje kwa kiasi kikibwa. Maghala hayo yamelengwa na makombora na kwa hiyo, masoko na mawakala wa maeneo hayo wameongeza bei ya unga, wakati ni chakula kinachotumiwa kila siku na familia nyingi za Yemen »