Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani vikali mashambulizi mjini Tripoli Libya

Baraza la usalama lalaani vikali mashambulizi mjini Tripoli Libya

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali mashambulio ya kigaidi dhidi ya balozi za Jamhuri ya Korea na Morocco yaliyofanywa mjini Tripoli Libya tarehe 12 na 13 mwezi huu wa April. Wajumbe hao pia wametuma salamu za rambirambi kwa familia za raia wawili wa Libya waliopoteza maisha katika mashambulizi hayo.

Wajumbe wamelaani vitendo vyote vya ghasia dhidi ya majengo ya kidoplomasia, vitendo ambavyo vinahatarisha maisha ya watu wasio na hatia na kuathiri kazi za kawaida za wanadiplomasia na maafisa wanaowakilisha nchi zao. Pia wamerejea kusisitiza kwamba ugaidi katika mfumo wowote ule ni tishio kubwa la amani na usalama na kwamba vitendo vyovyote ya kigaidi ni uhalifu na haukubaliki licha ya sababu yoyote iliyosababisha kufanyika na mtu yoyote au popote.

Wajumbe wamesisistiza haja ya kukabiliana kwa nia yoyote kwa kuzingatia mikataba ya Umoja wa Mataifa na wajibu chini ya sheria za kimatifa hasa za haki za binadamu , wakimbizi, na sheria za kibinadamu , vitisho vya amani ya kimataifa na usalama vinavyosababishwa na vitendo vya kigaidi.