Mratibu maalumu wa UM akutana na waziri mkuu wa Palestina

15 Aprili 2015

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati bwana Nikolay Mladenov amesema ametiwa moyo na uwajibikaji wa serikali ya Palestina kwa kuanza kutekeleza majukumu yake Gaza. Bwana Mladenov ameyasema hayo leo Jumatano baada ya kukutana na waziri mkuu wa Palestina Rami Hamdallah.

Na kuongeza kuwa wajibu walioanza kuutekeleza Gaza ni pamoja na kudhibiti wa uvukaji mpakani pamoja, kufanya mabadiliko katika huduma ya jamii na mchakato wa kuwajumuisha tena watu katika jamii.

Mratibu huyo amemuhakikishia waziri mkuu Hamdallah kuwa Umoja wa Mataifa upo tayari kusaidia juhudi zozote katika swala hilo na hasa ujenzi wa Gaza.

Ameongeza kuwa wakati huu ambapo kuna miradi mikubwa ya ujenzi wa nyumba na miundombinu itakuwa muhimu saana kwa Israel na wadau wote kufanya kazi pamoja na kuharakisha uingizaji wa vifaa vya ujenzi Gaza.

Pia ametumia fursa hiyo kutoa wito wa kuachiliwa kwa mapato yote ya kodi kwa kuzingatia mkataba wa Paris.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter