Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo haikwepeki katika kukuza amani na maendeleo: Ban

Michezo haikwepeki katika kukuza amani na maendeleo: Ban

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo kumefanyika mkutano ulioangazia umuhimu wa michezo katika kukuza maendeleo endelevu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya michezo kwa maendeleo na amani. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Sauti ya mtangazaji mashuhuri wa CNN Ralitsa Vassileva, ambaye ni mshereheshaji katika maadhimisho hayo yaliyojikita katika kuunganisha nguvu kwa ajili kwa ajili ya maendeleo endelevu kupitia michezo kwa wote.

Akihutubia katika maadhimisho hayo Rais wa baraza kuu la Sam Kutesa amesema michezo sio tu hukuza maendelo lakini pia hufundisha nidhamu na sheria, maadili ya kazi na hata kuujumuisha makundi maaluma kama walemavu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesisitiza umuhimu wa michezo akisema.

(SAUTI BAN)

"Naamini nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakati wakiandaa malengo endelevu yajayo watajumuisha michezo sio tu kwa ajili ya fya lakini pia amani na utulivu, upatanisho, malewano na heshima kwa wote.

Kwa upande wake Rais wa kamati ya kimataifa ya Olympiki IOC Thomas Bach amesema michezo hiyo ina misingi ya Umoja wa Mataifa kama vile uvumulivu, mshikamano na amani na hivyo inapaswa kutumiwa kote duniani kwa maendeelo na amani