Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito umetolewa kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto:

Wito umetolewa kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto:

Ukatili dhidi ya watoto ni hulka iliyosambaa na jumuiya ya kimataifa ni lazima ichukue hatua za haraka kukabiliana nao, umesema mjadala wa ngazi ya juu uliofanyika leo kwenye mkutano wa 13 wa uhalifu unaoendelea Doha.

Washiriki wa mjadala huo wamesema ili kufanikiwa vita dhidi ya ukatili wa watoto kuna umuhimu wa kuzingatia mikakati na hatua za Umoja wa Mataifa za kutokomeza tatizo hili, iliyopitishwa na baraza kuu mwezi Desemba mwaka jana kutokana na obi maalumu la serikali ya Thailand na Austria.

Akihudhuria mjadala huo Binti mfalme wa Thailand Bajrakitiyabha Mahidhol amesema mamilioni ya watoto wanatelekezwa, kutojaliwa na kuingia kwenye uhalifu duniani na kuwa wahanga wa mifumo ya haki na sharia.

(Sauti ya Binti mfalme BAJRAKITIYABHA)

“Sehemu kubwa ya ukatili huu inasalia kuwa mafichoni kutokana na uwoga , jamii kukubali ukatili na ukosefu wa njia salama na zinazoaminika ambazo wote watoto na watu wazima wanaweza kutoa taarifa za ukatili.”