Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwezi mmoja baada ya kimbunga Pam, Vanuatu bado inakabiliwa na changamoto za afya:WHO

Mwezi mmoja baada ya kimbunga Pam, Vanuatu bado inakabiliwa na changamoto za afya:WHO

Shirika la afya duniani WHO likishirikiana na wizara ya afya ya Vanuatu na wadau wengine wamepiga hatua kubwa katika kushughulikia mahitaji ya afya kwa watu Zaidi ya 160,000 walioathirika na kimbunga Pam.

Hata hivyo ikiwa ni mwezi mmoja sasa baada ya zahma hiyo kisiwani Vanuatu bado kuna changamoto nyingi za kiafya zilizosalia.

Kwa mujibu wa Dkt. Shin Young-soo, mkurugenzi wa WHO kanda ya Pacific Magharibi wa athari za kimbunga hicho zitadumu kwa muda mtrefu.

Ameongeza kuwa WHO itaendelea kushughulikia mahitaji ya haraka ya watu huku wakitumia janga hilo kama fursa ya kusaidia kujenga mifumo imara ya afya kisiwani Vanuatu.

WHO imekuwa ikifanya kazi bega kwa began a wizara ya afya ya kisiwa hicho kutathimini mahitaji na kuratibu misaada ya dharura ya kiafya.

Hadi sasa WHO kwa ushirika na wizara hiyo wameratibu kuwasili kwa timu 20 za kigeni za huduma za afya ambazo zimetoa huduma muhimu katika maeneo yaliyoathirika, wameahamisha wagonjwa, wamegawa dawa za dharura , tiba za kuhara na tembe za kusafisha 190,000 za kusafisha maji.

Pia kampeni ya chanjo ya surua imewafikia watoto 16,000 wa chini ya miaka mitano ambao pia walipewa dawa za minyoo na vitamin A.