Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaendelea kusafirisha raia wa kigeni kutoka Yemen:

IOM yaendelea kusafirisha raia wa kigeni kutoka Yemen:

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeendelea kusafirisha raia wa kigeni kutoka nchini Yemen. Jumanne wiki hii shirika hilo limefanya safari ya pili ya kuwahamisha kwa ndege raia wa nchi ya tatu kutoka Sana’a Yemen hadi Khartoum Sudan.

Watu 148 wamesafirishwa wakiwemo raia kutoka nchi 13 zikiwemo Albania, Bangladesh, Canada, Misri, Ethiopia, Ujerumani, Hungary, Uholanzi, Romania, Sweden, Tunisia, Uingereza na Marekani.

Operesheni hii ambayo inajumuisha pia utoaji wa huduma ya usafiri kutoka Khartoum na kuendelea makwao , inafuatia ile ya awali ya iliyofanywa na IOM kusafirisha watu wengine kutoka Sana’a hadi Khartoum Jumapili iliyopita ya tarehe 12 Aprili.