Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedetov ashtushwa na vifo vingine vya wahamiaji pwani Libya:

Fedetov ashtushwa na vifo vingine vya wahamiaji pwani Libya:

Bwana Yury Fedotov mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu (UNODC) amesema ameshtushwa na habari za kutisha za kuzama kwa mamia ya wahamiaji kwenye pwani ya Libya.

Ripoti za karibuni zinasema wahamiaji 400 wamekufa maji katika pwani hiyo wakati boti yao ilipozama.

Akiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa unoendelea Doha Qatar wa kuzuia uhalifu, bwana Fedotov amesema kuwasafirisha kinyemela wahamiaji ni kutumia vibaya hali waliyonayo ya madhila na kuupatia mtandao wa wahalifu faida kubwa.

(Sauti Fedotov)

“Wahamiaji 400 wameufa siku moja wakati boti yao ilipozama pwani ya Libya, ni tukio la siku moja. Wakati huohuo mtu katika upande mwingine wa Mediterranean amejipatia dola zingine milioni 1.5 kwenye akaunti yake ya bank. Huo ni uhalifu unaopaswa kushughulikiwa. Tunahitaji kulinda haki za wahamiaji , kuwasaidia, kuwalinda wanawake na hususan watoto wakiwemo wale wanaosafiri bila kusizndikizwa na mtu.

Pia amezungumzia umuhimu wa kushughulikia chanzo na sababu za kusafirisha kinyemela wahamiaji.

(Sauti ya FEDOTOV)

“Hii ni muhimu saana na ndio maana kauli mbiu ya mkutano wa Doha ni ya maanakwa sababu utawala wa sharia na mifumo ya haki vinashabihiana vikisaidiwa na maendeleo endelevu. Wakati huohuo maendeleo endelevu ynaweza kuwa sababu muhimu ya kuboresha mifumo ya haki na utawala wa sheria.”