Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je wafahamu athari za kujifungua kwa njia ya upasuaji?

Je wafahamu athari za kujifungua kwa njia ya upasuaji?

Kujifungua kwa upasuaji au operesheni kumekuwa mtindo, idadi ya operesheni ikiongezeka katika nchi zote duniani, na kuwatia wasiwasi watalaam wa Shirika la Afya Duniani WHO.

Kwa mujibu wa WHO, upasuaji unapaswa kufanyika iwapo tu mjamzito au mtoto aliye tumboni ana tatizo la kiafya, vinginevyo, upasuaji unaweza kuwa na athari pindi unapofanyika na hata baadaye.

Je ni vigezo gani vinapaswa kuzingatiwa, na athari ni zipi? Basi ungana na Priscilla Lecomte katika mahojiano yake na Daktari James Kiarie kutoka Kenya ambaye ni mratibu wa timu ya afya ya uzazi ya WHO. Hapa Dokta Kiarie anaanza kwa kulezea kwanini WHO imekuwa na wasiwasi juu ya mwelekeo huo.