Baraza la usalama lalaani mauaji ya mlinda amani Haiti

Baraza la usalama lalaani mauaji ya mlinda amani Haiti

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio dhidi ya gari la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH, mnamo April 13 ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani raia wa  Chile.

Wajumbe wa baraza la usalama wameelezea pia rambirambai zao za dhati kwa familia za mlinda amani huyo aliyefariki, serikali ya Chile na watu wa nchi hiyo na MINUSTAH .

Wametaka uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo utakaotoa ukweli halisi.