Skip to main content

Libya yatakiwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

Libya yatakiwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

Baraza la usalama limeitaka Libya kukubali mpango wa muundo wa serikali ya Umoja wa kitaifa ili kukomesha janga la kisiasa, usalama na kitaasisi.

Taarifa ya baraza hilo inakariri mkutano wa viongozi wa kisiasa nchini Algeria Aprili 13 unaowezeshwa na Umoja wa Mataifa ambapo mkutano mwingine unatarajiwa kufanyika Aprili 15 nchini Morroco.

Wajumbe wa baraza hilo wanasisitiza kuwa suluhu la kijeshi haliwezi kukomesha machafuko , hivyo kutaka  pande zote nchini Libya kusitisha uhasama na kuandaa mazingira ya usalama kwa ajili ya majadiliano jumuishi.