Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magari yasiyokidhi viwango vya usalama huuzwa nchi maskini:Ripoti

Magari yasiyokidhi viwango vya usalama huuzwa nchi maskini:Ripoti

Idadi kubwa ya vifo na majeruhi kutokana na ajali duniani ingaliweza kuepuka kila mwaka iwapo serikali zingalizingatia viwango vya usalama wa magari kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa Mataifa. Hiyo ni imo kwenye matokeo ya tafiti ya hivi karibuni ya mpango wa tathmnini ya magari mapya duniani Gobal NCAP kama anavyofafanua Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Utafiti huo uliohusisha pia tume ya umoja wa mataifa ya uchumi barani Ulaya, UNECE, umebaini kuwa mamilioni ya magari yauzwayo nchi zenye vipato vya chini hayakidhi viwango vya majaribio ya ajali kwa upande wa mbele na pembeni.

Mathalani katika jaribio moja gari liligongeshwa kwa mbele katika mwendo wa kiilometa 64 kwa saa na halikupata alama hata moja ikimaanisha kuwa iwapo linapata ajali inaweza kuwa mbaya na kusababisha vifo.

Katibu Mtendaji wa UNECE Christian Friis Bach amesema haikubaliki magari yanayouzwa nchi maskini kwa makusudi hayakidhi viwango vya usalama kama yala yanayozwa nchi zilizoendelea.

Amevitaka viwanda vya magari kuhakikisha viwango vya usalama vinatumika kwa magari yote duniani kote na kutaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataiaf kuridhia na kutekeleza viwango vya usalama barabarani na muundo wa mgari.

Umoja wa Mataifa unasema kila mwaka watu zaidi ya Milioni Moja hufariki dunia kwenye ajali za barabarani huku Mililoni 50 wakijeruhiwa ambapo asilimia 80 ya vifo ni katika nchi za vipato vya chini.