Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Singapore na UM zajadili uimarishaji wa majeshi ya kiraia:OCHA

Singapore na UM zajadili uimarishaji wa majeshi ya kiraia:OCHA

Wizara ya ulinzi ya Singapore na ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA zinaendesha mkutano wa kimataifa wa masuala ya kibinadamu kuhusu uratibu wa majeshi ya kiraia katika masuala ya kibinadamu kwenye kituo cha Changi Singapore kuanzia leo 13 hadi 15 April 2015.

Jukwaa hilo litasaidia kuunda mjadala na ajenda za mkutano wa dunia wa masuala ya kibinadamu utakaofanyika Istanbul Uturuki mwezi Mei mwaka 2016.

Jukwaa hilo la kimataifa linataka kuweka mapendekezo ya kuimarisha uratibu wa uwezo na uwepo wa jeshi la kiraia katika kukabiliana na majanga katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Zaidi ya watunga sera na wataalamu kutoka mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa , mashirika ya kikanda, na yasiyo ya kiserikali NGO’s , pamoja na mamlaka za udhibiti wa majanga vikiwemo vyombo vya ulinzi kutoka nchi Zaidi ya 25 wawanahudhuria jukwaa hili la siku tatu.