Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataka vyanzo vya maji chini ya ardhi vilindwe

Wataka vyanzo vya maji chini ya ardhi vilindwe

Shirika la kilimo na chakula FAO, lile la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, kwa kushirikiana na taasisi ya kimatifa ya wataalamu wa maji chini ya radhi hydrolojia, yametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushughulika ongezeko la dharura la kupungua kwa vyanzo vya rasilimali za maji ardhini.

Angalizo hili linakuja kulekea mkutano wa saba wa dunia mjini Daegu na Gyeongbuk Korea Kusini juma lijalo,  ambapo mashirika hayo yameshauri kuundwa kanuni zitakazotumiwa na serikali kwa ajili ya udhibiti bora wa maji chini ya ardhi.

Mkakati wa kimataifa wa mwaka 2030 unataka juhudi za pamoja miongoni mwa serikali na jamii ya kimataifa katika kuhakiisha matumizi endelevu ya maji ya chini ya ardhi.

Taarifa ya mashirika hayo inasema kuwa sera ya  maji ardhini imekuwa haitiliwi maanani jambo linalosababisha kupungua na uharibifu wa maji hayo.  Kutozingatiwa kwa maji ardhini  kumeongezeka mara tatu katika kipindi cha nusu karne iliyopita imeongeza taarifa hiyo.