Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu kuchunguza madai ya kaburi la pamoja DRC

Ofisi ya haki za binadamu kuchunguza madai ya kaburi la pamoja DRC

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeelezea wasiwasi wake baada ya kupokea ripoti kuhusu uwepo wa kaburi la pamoja la watu 421 kwenye manispaa ya Maluku, iliyoko jimbo la Kinshasa ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Ravina Shamdasani amesema ofisi hiyo inaendelea na uchunguzi kuhusu suala hilo kwa ushiriano na mamlaka za serikali, ikieleza. kuendelea pia na uchunguzi huru kwenye eneo husika, kwa kuhoji familia za wahanga na mashahidi.

Ofisi ya haki za binadamu nchini DRC imesema itaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha uchunguzi unafanyika kwa njia wazi na huru.