Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 130 kujadili uhalifu huko Doha

Nchi 130 kujadili uhalifu huko Doha

Mjini Doha, nchini Qatar, kongamano la 13 la Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia uhalifu na sheria ya uhalifu litaanza jumapili, huku nchi zaidi ya 130 zikitarajiwa kushiriki. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Kwa mujibu wa Dimitri Vlassis, Katibu Mtendaji wa kongamano hilo, ni takribani washiriki 4,000 watahudhuria kongamano hilo ambapo wakati huu likiadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, Katibu Mkuu Ban Ki-moon atahudhuria kwa mara ya kwanza.

Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Vlassis amesema tayari mazungumzo ya awali yamefanyika kuhusu azimio la mwisho la kongamano hilo, akisema rasimu hiyo ni nzuri kuliko zingine.

“ Inatambua na inamulika umuhimu wa kujumuisha maswala ya kuzuia uhalifu na sheria ya uhalifu kwenye ajenda ya Umoja wa MAtaifa kwa ujumla, hasa wakati huu jamii ya kimataifa inazungumzia uundwaji wa malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya maendeleo ya baada ya 2015”