Mashirika ya kiraia yana nafasi kubwa katika SDG

9 Aprili 2015

Kuelekea mkutano wa kimataifa wa ufadhili wa fedha kwa maendeleo huko Addis Ababa Ethiopia mwezi Julai mwaka huu, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema mashirika ya kiraia yana nafasi kubwa ya kufanikisha maendeleo endelevu, SDGs yatakayoanza kutekelezwa baadaye mwaka huu.

Kutesa amesema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu rais wa baraza hilo Balozi Nicholas Emiliou, wa Cyprus kweney mashauriano ya pili na mashirika ya kiraia kuhusu juu ya ufadhili wa fedha kwa maendeleo jijini New York.

Mathalani amesema malengo pendekezwa 17 ya SDG yana matarajio makubwa sana katika kubadilisha jamii kiuchumi na kijamii na kulinda sayari ya dunia lakini changamoto ni ufadhili wa kifedha pamoja na stadi

Ametolea mfano suala la kutokomeza umaskini linahitaji ufadhili wa ziada wa dola bilioni 66 kila mwaka huku ule wa miundombinu kama vile nishati na usafirishaji kwa ujumla ukihitaji kati ya dola Trilioni Tano hadi Saba kwa maka.

Hivyo amesema ili kufanikisha lengo hilo ni lazima kujumuisha rasilimali, stadi, ufahamu na mawazo bunifu kutoka jamii nzima ambapo ndipo mashirika yasiyo ya kiseriakli yanapokuwa na dhima muhimu.

Kwa mantiki hiyo Kutesa amesema kuelekea mkutano wa Addis Ababa ni vyema kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kupitia mchakato mzima wa ufadhili wa fedha kwa maendeleo

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter