Skip to main content

Rasimu ya sheria dhidi ya ugaidi na kashfa inadidimiza haki ya kujieleza:Zeid

Rasimu ya sheria dhidi ya ugaidi na kashfa inadidimiza haki ya kujieleza:Zeid

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu ameitaka serikali ya Malaysia kutupilia mbali mapendekezo katika rasimu  ya sheria dhidi ya ugaidi na kashiifa, akisema zinakandamiza zaidi haki za binadamu. Taarifa kamili na John Kibego.(Taarifa ya John Kibego)

Zeid Ra’ad Al Hussein ameonya kuwa, marekebisho yaliyopendekezwa katika sheria dhidi ya kashifa ya 1948 yaleta vipengele vinavyokandamiza haki ya kujieleza na kutoa maoni, ikiwa ni kinyume kabisa cha katiba ya nchi hiyo na wajibu wake kwa sheria za kimataifa kuhusu haki za bihytnadamu.

Ametamaushwa na sheria iliyopitishwa na bunge la chini Jumanne wiki hii, ambayo inasaka miongoni mwa mengine kifungo cha muda usiyobainika, kwa washukiwa wa ugaidi bila kuwapelekwa mahakamani na wala kujali wanaokiuka haki zao.

Wakati huo huo, sheria dhidi ya kashifa bungeni ina vipengele vinavyoongeza adhabu ikiwemo kifungo cha miaka 20 gerezani, na kubana safari za nje kwa baadhi ya watu.

Tangu 2014, angalau watu 78 wamechunguzwa au kufunguliwa mashitaka ya kashifa. Wengine 36 nao wamechunguzwa au kufunguliwa mashitaka hayohayo mnamo kwaka huu peke.

Bwana Al Hussein amesema, Malaysia imekaidi kabisa wito wa muda mrefu wa Ofisi ya  Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kurekebisha sheria hiyo mbaya na badala yake inaifanya kuwa mbaya zaidi.