Skip to main content

Baraza la Usalama lajadili hali nchini Mali

Baraza la Usalama lajadili hali nchini Mali

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili hali nchini Mali na kufuatiwa na mashauriano kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA. Amina Hassan na maelezo kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Herve Ladsous anasema suluhu la mgogoro linasalia kuwa makubaliano kupitia mazungumzo kati ya pande kinzani.

Amesema nchi za ukanda wa Magharibi mwa Afrika zina jukumu muhimu.

(SAUTI LADSOUS)

"Ni muhimu kwa nchi za ukanda huo na washirika wa Mali waendelee kuunga mkono MINUSMA na wafanyakazi wake ili kwezesha ujumbe huu kutekeleza majukumu yake hususani ni katika misafara ya ugawaji misaada kupitia nchi jirani".

Kwa upande wake mwakilishi wa Mali katika Umoja wa Mataifa Sekou Kasse ameliambia baraza la usalama kuwa WATU WA Mali wamechoka na machafuko, wanahitaji utu na heshima kwa kurejea katika amani nchini mwao.